Sabri Brothers

Picha ya bendi ya Sabri Brothers
Picha ya bendi ya Sabri Brothers

Sabri Brothers (kwa Kipanjabi, Kiurdu: صابری برادران) ni bendi ya muziki kutoka nchini Pakistan ambayo hutumbuiza Sufi qawwali na wana mahusiano ya karibu na Chishti Order. Wanajulikana kama mabalozi wanaohamia Pakistan.

Bendi hiyo ilianzishwa na Maqbool Ahmed Sabri akiwa na umri wa miaka 11 ambayo ilijulikana kama Bacha Qawwal Party na baadaye, kaka yake mkubwa Ghulam Farid Sabri alijiunga kwa msisitizo wa baba yao kuwa kiongozi wa kikundi hicho na bendi hiyo ilijulikana kama Sabri Brothers.[1] Walikuwa wasanii wa kwanza kabisa wa Qawwali kutumbuiza Qawwali huko Marekani na nchi zingine za Magharibi, pia walikuwa wasanii wa kwanza kabisa wa Asia kutumbuiza katika Jumba la Carnegie la New York mnamo 1975.[2] Sabri Brothers wamefanya maonyesho kadhaa ya qawwali ulimwenguni.

  1. MAQBOOL AHMED SABRI, YADGAAR INTERVIEW ALONG HIS DAUGHTER AMEEMA BAJI WITH FARAH MADAM, iliwekwa mnamo 2021-04-10
  2. Chris Menist (2011-10-12). "Maqbool Sabri obituary". the Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-04-10.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search